Chomeka flash iliyo haribika
kwenye computer yako na hakikisha imesoma, na usichomeke kifaa kingine chochote
zaidi ya flash yako iliyo haribika tu. Baada ya hapo fuata hatua zifuatazo:-
1.
Fungua CMD
kwa kubofya start key + R kisha
andika cmd alafu bonyeza Enter CMD itafunguka.
2.
Andika kwenye cmd diskpart kisha bofya Enter,
itakuuliza kubali kwa kubonyeza OK
kisha endelea kufuata hatua…
3.
Andika list
disk kisha bofya Enter, hapo
utaona local disk za computer yako pamoja na flash uliyo chomeka.
4.
Angalia flash yako ni namba ngapi kisha
andika select disk kisha ruka nafasi
andika namba ya disk ilipo flash yako kisha bofya Enter,mara nyingi huwa ni disk 1 kwaiyo utaandika select disk 1.
5.
Baada ya hapo andika clean kisha bofya Enter.
6.
Andika create
partition primary kisha bonyeza Enter.
7.
Kisha andika active alafu utabofya Enter.
8.
Baada ya hapo utaandika select partition 1 kisha bofya Enter.
9.
Mwisho utamalizia kwa kuandika format fs=fat32 kisha bofya Enter.
Ukimaliza kufuata hatua zote
hizi subiri kwa mda kadhaa hadi itakapo fika asilimia mia flash yako itakua nzima unaweza kuichomoa na kuifanyia
matumizi yako