:::: MENU ::::
  • Suitable for all screen sizes

  • Easy to Customize

  • Customizable fonts.

Tuesday 27 March 2018




Chomeka flash iliyo haribika kwenye computer yako na hakikisha imesoma, na usichomeke kifaa kingine chochote zaidi ya flash yako iliyo haribika tu. Baada ya hapo fuata hatua zifuatazo:-
1.    Fungua CMD kwa kubofya start key + R kisha andika cmd alafu bonyeza Enter CMD itafunguka.
2.    Andika kwenye cmd diskpart kisha bofya Enter, itakuuliza kubali kwa kubonyeza OK kisha endelea kufuata hatua…
3.    Andika list disk kisha bofya Enter, hapo utaona local disk za computer yako pamoja na flash uliyo chomeka.
4.    Angalia flash yako ni namba ngapi kisha andika select disk kisha ruka nafasi andika namba ya disk ilipo flash yako kisha bofya Enter,mara nyingi huwa ni disk 1 kwaiyo utaandika select disk 1.
5.    Baada ya hapo andika clean kisha bofya Enter.
6.    Andika create partition primary kisha bonyeza Enter.
7.    Kisha andika active alafu utabofya Enter.
8.    Baada ya hapo utaandika select partition 1 kisha bofya Enter.
9.    Mwisho utamalizia kwa kuandika format fs=fat32 kisha bofya Enter.
Ukimaliza kufuata hatua zote hizi subiri kwa mda kadhaa hadi itakapo fika asilimia mia flash yako itakua nzima unaweza kuichomoa na kuifanyia matumizi yako
A call-to-action text Contact us